Jun 13, 2021 06:36 UTC
  • Mwandishi wa Marekani adai nyambizi za siri za Russia ni tishio kwa Marekani

Shirika la vyombo vya habari la Forbes la Marekani limedai kuwa, nyambizi za siri za Russia ni tishio Marekani na nchi za Magharibi.

Shirika la habari la Sputnik la Russia limemnukuu Loren Thompson, mwandishi wa makala wa shirika la vyombo  vya habari la Forbes la Marekani akidai kwamba nyambizi za siri za Russia ni tishio na ni "tatizo la kishetani" kwa Magharibi.

Mwandishi huyo mwandamizi wa makala za Forbes pia amesema, Marekani inaweza kuzipa nchi za Ulaya njia ya bei rahisi ya kujihami kutokana na hatari za nyambizi za siri za Russia.

Amedai kuwa, njia hiyo rahisi ni kulitia nguvu jeshi la nchi za Magharibi NATO na kuimarisha uwezo wa viwanda vya nchi za Ulaya. Amesema, inaonekana mambo hayo hata hayahitajii kutengewa bajeti mpya kwani bajeti yake ipo tayari.

Ugomvi baina ya Russia na Marekani

 

Ameongeza kuwa, sasa hivi nchi za Ulaya hazina uwezo wa kugundua nyambizi za siri za Russia. Hata hivyo amesema, Marekani ina ndege aina ya P-8 Poseidon za kugundua nyambizi na inaweza kuwapa taarifa hizo waitifaki wake.

Ikumbukwe kuwa, miaka minane iliyopita ya utawala wa Donald Trump, rais huyo wa Marekani alifuata siasa za kujikumbikizia kila kitu upande wake, hivyo alivuruga mno uhusiano wa Washington na hata waitifaki wake wa karibu mno kama vile Uingereza na nchi za Ulaya.

Trump alisema kuwa, nchi za Ulaya zinainyonya Marekani kupitia gharama za jeshi la NATO na alitaka nchi za Ulaya zinunue kwa gharama ya juu msaada wa Marekani ndani ya NATO. Hata hivyo siasa za rais wa hivi sasa wa Marekani, Joe Biden ni kinyume kikamilifu na za Trump kuhusu suala hilo.