Jun 13, 2021 07:05 UTC
  • Umoja wa Ulaya watoa onyo kali kwa Uingereza

Wakuu wa Umoja wa Ulaya wametoa onyo kali kwa waziri mkuu wa Uingereza na kumtaka aheshimu ahadi za London ndani ya Brexit.

Bi Ursula von der Leyen na Charles Michel wakuu wa kamisheni na baraza la Ulaya wakiwa nchini UIngereza kushiriki kwenye kikao cha kukndi G7 wamekutana na waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johns na kumuonya kuhusu hatari za kutotekeleza ahadi zake serikali ya London kuhusu makubaliano ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya maarufu kwa jina la Brexit.

Wakuu hao wa kamisheni na baraza la Ulaya wamemuonya Boris Johnson kwa kumwambia kuwa, Umoja wa Ulaya hautokaa kimya kama London haitotekeleza ahadi zake ndani ya Brexit.

Boris Johnson, waziri mkuu wa Uingereza

 

Mzozo baina ya Umoja wa Ulaya na UIngereza umeongezeka hasa kutokana na London kutoheshimu protokali zinazohusiana na Ireland Kaskazini. Umoja wa Ulaya umetishia kwamba kama Uingereza haitoheshimu makubaliano, basi umoja huo utaiwekea vikwazo London.

Masoko ya fedha ya Umoja wa Ulaya yamekuwa chini ya mashinikizo tangu Uingereza ijitoe kwenye umoja huo kiasi kwamba wafanyabiashara wengi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakumbwa na matatizo mbalimbali katika miamala yao ya kifedha.

Mwaka 2016 Uingereza iliitisha kura ya maoni ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya. Tarehe 29 Machi 2017 mchakato wa kujitoa London kwenye umoja huo ulianza rasmi.

Hatimaye tarehe 31 Januari 2020, Uingereza ilijitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya huku kukiwa na mambo mengi yenye utata yasiyotatuliwa kama suala la Ireland Kaskazini.

Tags