Jun 13, 2021 11:56 UTC
  • Dakta Tedros Adhanom Gebreyesus
    Dakta Tedros Adhanom Gebreyesus

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameitaka China ishirikiane katika kutafiti channzo cha maambukizi ya kirusi cha corona.

Dakta Tedros Adhanom Gebreyesus amesema, ni vyema China ikashirikiana na kuwa wazi kuhusu chanzo na asili ya mambukizi ya corona duniani. Dakta Adhanom ameongeza kuwa, tayari WHO imejiandaa kwa ajili ya hatua zinazofuata za kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha kutokea maambukizi ya corona, ni kwamba jambo hili ni moja kati ya kadhia zilizojadiliwa katika kikao cha jana cha wakuu wa kundi la G-7.   

Idara ya intelijinsia za Marekani sasa zimejiekeleza kwenye masuala mawili kuhusu chanzo cha maambukizi ya Covid-19; ambazo ni kwamba, ugonjwa huo ni matokeo ya kugusana binadamu na mnyama aliyeambukizwa au ni jambo lililotengenezwa ndani ya maabara.   

Kirusi cha corona kinachosababisha ugonjwa wa Covid-19  kwa mara ya kwanza kiliripotiwa katikati ya mwezi Disemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan katikati ya China.  Aawali ugonjwa huo ulitajwa kuwa ni Homa ya Mapafu (pneumonia) lakini baadaye Kamisheni ya Taifa ya Afya ya China ilitangaza rasmi maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo. 

Mji wa Wuhan, China kuliporipotiwa kwa mara ya kwanza maambukizi ya corona 

Takwimu za kimataifa  zinaonyesha kuwa, hadi sasa watu milioni 176 na 423,545 wameambukizwa corona duniani; na milioni tatu na 810,993 miongoni mwao wamefariki dunia kwa ugonjwa huo.