Jun 14, 2021 08:17 UTC
  • Wapinzani wa utawala wa kijeshi Myanmar watangaza mshikamano na Waislamu wa Rohingya

Wapinzani wa utawala wa kijeshi nchini Myanmar wameanzisha kampuni ya kuonyesha mshikamano wao na Waislamu wa jamii ya Rogingya wanaodhulumiwa na kukandamizwa nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza kushuhdiwa tukio kama hilo katika nchi ya Myanmar ambako Mabudha wenye misimamo mikali wamekuwa wakishirikiana na jeshi la nchi hiyo kuwakandamiza Waislamu hao waliowachache.

Jana Jumapili wapinzani wa utawala wa kijeshi wa Myanmar walichapicha picha zao wakiwa wamevalia nguo za rangi nyeusi na kuinua juu vidole viitatu kama ishara ya mapambano, chini ya kaulimbiu inayosema: "kwa ajili ya Rohingya".

Harakati hii ya watu wa Myanmar kuonesha himaya na mshikamano wao na Waislamu wa jamii ya Rohingya inaonekana kwenda kinyume na hali ilivyokuwa hapo kabla ambapo kulitaja jina la Rohingya pekee lilikuwa kosa la jinai.

Maelfu ya Waislamu wa Rohingya wameuawa Myanmar

Tarehe Mosi ya mwezi huu wa Februari jeshi la Myanmar lilitangaza kudhibiti madaraka ya nchi baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi nchini Myanmar, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo ambayo ilizua hofu ya kutokea mapinduzi.

Gazeti la The Observer limeandika kuwa, Baraza la Kijeshi la Myanmar lililotwaa madaraka ya nchi mwaka 1962 lilieneza chuki dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya kama wenzo wa kuimarisha nafasi yake baina ya wanachi na likaanza operesheni ya mauaji ya kimbari ambayo yalishadidi zaidi mwaka 2017 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.

Itakumbukwa kuwa wimbi jipya la mauaji, mashambulizi na ubakaji wa jeshi la Myanmar katika mkoa wa Rakhine kuwalenga Waislamu wa Rohingya, lilianza tarehe 25 Agosti mwaka 2017 ambapo zaidi ya Waislamu elfu sita waliuawa na wengine elfu nane kujeruhiwa. Aidha zaidi ya Waislamu wengine milioni moja wa jamii hiyo walilazimika kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh.

Tags