Jun 17, 2021 12:33 UTC
  • Kremlin: Mapatano ya JCPOA yanaweza kurejea kama awali

Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) ameashiria mazungumzo kati ya Marais wa Russia na Marekani kuhusu kadhia ya Iran katika kikao cha Geneva na kusema kuwa: kuna matarajio mapatano ya JCPOA yakarejea kama yalivyokuwa awali.

Dymitry Peskov amesema kuwa, Rais Vladimir Putin wa Russia na mwenzake wa Marekani Joe Biden katika kikao chao cha jana huko Geneva walijadili kadhia ya mapatano ya JCPOA; ambapo Moscow imesema, inataraji kuwa mapatano hayo ya nyuklia yatarejea katika hali yake ya awali. 

Kuhusu hitilafu na tofauti zilizopo baina ya Moscow na Washington kuhusiana na mapatano ya JCPOA, Msemaji huyo wa Ikulu ya Russia amesema: kuna mipango maalumu kuhusu suala hilo. Muhimu ni kuwa mapatano ya JCPOA yanaweza kurudi kama yalivyokuwa huko nyuma; yapo matarajio na harakati za kurekebisha hali ya sasa," amesema Peskov wakati alipohojiwa na redio ya Moscow leo Alkhamisi.  

Marais Joe Biden na Vladimir Putin wa Marekani na Russia kwa utaratibu 

Katika upande mwingine, Msemaji huyo wa Kremlin ameshiria masuala mengine yaliyojadiliwa na Marais wa Russia na Marekani katika kikao cha Geneva. Amesema, mazungjmzo kati ya jeshi la Russia na Marekani huko Syria yana umuhimu na yanapaswa kuungwa mkono. 

Itakumbukwa kuwa, Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump tarehe 8 Mei mwaka 2018 alijitoa kivyake na bila sababu katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kuamuru kurejeshewa Iran vikwazo vilivyokuwa vimesitishwa licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuheshimu kikamilifu vipengee vya mapatano hayo.  Aidha viongozi wa serikali ya Joe Biden wamekiri mara kwa mara juu ya kugonga mwamba vikwazo hivyo vya mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi dhidi ya Iran hata hivyo hadi sasa  wameshindwa kuchukua hatua za  kivitendo za kurejea kwenye mapatano hayo.