Jun 19, 2021 02:24 UTC
  • Idadi ya wakimbizi haijapungua licha ya kuweko sheria kali za corona duniani

Idadi ya wakimbizi duniani haijapungua licha ya sheria kali za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 zinazoendelea kuchukuliwa na nchi mbalimbali duniani.

Hayo yalisemwa jana Ijumaa na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi, Filippo Grandi, ambaye ameongeza kuwa, licha ya mipaka ya nchi mbali mbali kufungwa na licha ya mataifa ya dunia kuweka sheria kali za kukabiliana na corona, lakini pamoja na hayo, masuala kama vita, machafuko na uvunjaji wa haki za binadamu hayajaruhusu kupungua idadi ya wakimbizi duniani. 

Kwa mujibu wa  Filippo Grandi, karibu watu milioni tatu walilazimika kukimbia makazi yao katika kona mbalimbali za dunia mwaka uliopita wa 2020 kutokana na vita, machafuko na uvunjaji wa haki za binadamu. 

Wahanga wakuu wa janga la wakimbizi ni wanawake na watoto wadogo

 

Ametoa ufafanuzi zaidi kwa kusema, mapigano, majanga ya kimaumbile na mabadiliko ya hali ya tabianchi yalisababisha ongezeka la wakimbizi mwaka 2020 katika maeneo kama ya Msumbiji, Tigray Ethiopia na eneo la Sahel la Afrika. Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi, maeneo hayo aliyoyataja ndiyo yalikuwa wazalishaji wakubwa wa wakimbizi mwaka jana na kiujumla dunia ilishuhudia ongezeko la wakimbizi karibu milioni 3 mwaka huo.

Takwimu zinaonesha kuwa, hadi mwaka jana 2020, idadi ya wakimbizi duniani ilikuwa ni zaidi ya milioni 5 na laki 7 wa Kipalestina, milioni 3 na laki 9 wa Venezuala, milioni 20 na laki 7 wa nchi nyingine duniani, wote hao wanaishi nje ya mipaka ya nchi zao. Ripoti hiyo imeongeza kwamba, hadi mwaka jana kulikuwa na wakimbizi milioni 48 wa ndani ya mipaka ya nchi zao.

Tags