Jun 21, 2021 06:51 UTC
  • Global Times: Marekani ndiyo mashine ya mauaji ya umati duniani

Gazeti la lugha ya Kiingereza la Global Times limetoa takwimu zinazohusiana na historia ya mauaji yanayofanywa na wanajeshi wa Marekani nje ya nchi hiyo hususan katika eneo la Asia Magharibi ikiwemo Afghanistan na kusema kuwa, Washington ndiyo mashine ya mauaji ya umati duniani.

Gazeti hilo limesema kuwa, Marekani ina wanajeshi katika zaidi ya nchi 150 duniani na inakadiriwa kuwa, maafisa laki moja na 65,000 wa kijeshi wa Marekani wanafanya kazi zao nje ya nchi hiyo. Si hayo tu, lakini pia Marekani ina mamia ya kambi za kijeshi nje ya mipaka yake, na hakuna bara la dunia lisilo na kambi za kijeshi za Marekani.

Gazeti hilo limegusia pia ripoti ya kila mwaka ya wizara ya ulinzi ya Marekani na kusema kuwa, wiki iliyopita, Pentago (wizara ya ulinzi wa Marekani) ilitoa ripoti yake ya kila mwaka kuhusu mauaji ya raia yanayofanywa na wanajeshi wa Marekani nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Ripoti hiyo ilikiri kwamba operesheni za kijeshi za Marekani katika nchi za Afghanistan, Somalia na Iraq mwaka jana ziliua makumi ya raia wasio na hatia.

Katika jinai kubwa zilizofanywa na Marekani dhidi ya binadamu duniani ni mashambulizi yake ya nyuklia ya Hiroshima na Nagasaki huko Japan yaliyoua kwa umati watu kwa miaka mingi

 

Hali imekuwa ni hiyo hiyo kwa miaka mingi sasa. Kwa mfano Marekani ilikiri kuua raia 63 na kujeruhiwa 22 wengine katika nchi mbalimbali hasa Syria na Yemen baina ya mwaka 2017 na 2019.

Kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya ulinzi ya Marekani, tangu mwaka 2017, raia 773 wasio na hatia wameuliwa katika operesheni za kijeshi za Marekani na 335 wengine wamejeruhiwa.

Wataalamu huru na taasisi zisizo zisizo za kiserikali duniani zinasema kuwa, idadi ya raia wanaouliwa kidhulma na wanajeshi wa Marekani katika kona mbalimbali ulimwenguni ni kubwa mno ikilinganishwa na hiyo ambayo Marekani inakiri katika ripoti zake za kila mwaka.