Jun 23, 2021 02:29 UTC
  • Utafiti: Askari wa US wanaojiua ni wengi zaidi ya wanaokufa vitani

Utafiti mpya umefichua kuwa, idadi ya askari wa Marekani na maveterani wa kijeshi wa nchi hiyo wanaoaga dunia kwa kujitoa uhai ni mara nne zaidi ya wanajeshi wa dola hilo la kibeberu wanaouawa vitani katika vita vinavyoanzishwa na Washington kila uchao tokea Septemba 11 mwaka 2001.

Ripoti ya utafiti huo iliyopewa anuani ya Gharama za Mradi wa Vita (Costs of War Project) inaonesha kuwa, tokea yajiri mashambulizi ya Septemba 11 hadi sasa, wanajeshi na maveterani 30,177 wa Marekani wamejiua kutokana na msongo wa mawazo, ikilinganishwa na 7,057 walioaga dunia katika 'medani ya vita.'

Utafiti huo umebainisha kuwa, miongoni mwa sababu za ongezeko la kujitoa uhai wanajeshi wa Marekani, ni kupungua kwa imani ya Marekani kwa vita vinavyoanzishwa na Washington kwa kisingizio cha mashambulio ya Septemba 11.

Katika mashambulizi hayo ya mwaka 2001 wanachama 19 wa kundi la kigaidi la al Qaida waliteka nyara ndege nne za abiria na kuzitumia katika kushambuulia ya maeneo kadhaa ya Marekani likiwemo jengo la Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo, Pentagon. Karibu watu 3,000 waliuawa katika hujuma hiyo. 

Baada ya mashambulizi hayo Marekani ilizishambulia nchi za Iraq na Afghanistan kwa kisingizio cha kukabiliana na ugaidi, na mpaka sasa inaendelea kuzishambulia nchi hizo na nyingine tofauti duniani zikiwemo za Kiafrika kwa kisingizio hicho hicho.

Msongo wa mawazo unavyowasumbua askari wa US

Utafiti huo mpya umeonesha kuwa, asilimia 60 ya maveterani wa kijeshi wa US wanaamini kuwa, utawala wa George W. Bush ambao ulianzisha hujuma hizo za eti kuwasaka waliohusika na matukio ya Septemba 11 haukuwa na malengo ya wazi na ya kistratajia ya kuivamia Afghanistan.

Haya yanaripotiwa siku chache baada ya gazeti la lugha ya Kiingereza la Global Times kutoa takwimu zinazohusiana na historia ya mauaji yanayofanywa na wanajeshi wa Marekani nje ya nchi hiyo hususan katika eneo la Asia Magharibi ikiwemo Afghanistan na kusema kuwa, Washington ndiyo 'mashine ya mauaji ya umati duniani.'

 

Tags