Jul 23, 2021 02:31 UTC
  • Lavrov: Russia haina mpango wa kutuma wanajeshi Afghanistan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesisitiza kuwa, nchi hiyo haina mpango wa kutuma wanajeshi Afghanistan.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la habari la Interfax, Sergei Lavrov amesema kuwa Moscow haijachunguza suala la kutuma wanajeshi huko Afghanistan au kufanya mashambulizi dhidi ya makundi ya kigaidi nchini humo. 

Lavrov ameongeza kuwa, Moscow haijatoa pendekezo kwa Marekani kwa ajili ya kutumiwa kambi za kijeshi za Russia huko Tajikistan na Kyrgyzstan chini ya kivuli cha matukio ya hali ya sasa huko Afghanistan. 

Imeelezwa kuwa katika wiki za karibuni Russia iliihakikishia Tajikistan, moja ya nchi zenye mpaka wa pamoja na Afghanistan, kwamba itaisaidia kukabiliana na vitisho vya kiusalama kutoka nchi hiyo na kuimarisha ulinzi  katika mipaka ya Tajikistan  na Afghanistan. 

Kundi la wanamgambo wa Taliban la nchini Afghanistan limezidisha mashambulizi yake nchini humo sambamba na kuondoka wanajeshi vamizi wa Marekani huko Afghanistan. Wiki kadhaa zilizopita kundi hilo lilidhibiti maeneo mbalimbali ya Afghanistan suala lililowafanya viongozi wa serikali ya Kabul na baadhi ya nchi za kanda hiyo na kimataifa kutoawito wa kusitishwa mashambulizi hayo ya Taliban. 

Wanamgambo wa kundi la Taliban wa nchini Afghanistan 

 

Tags