Jul 23, 2021 11:15 UTC
  • Lavrov: Magharibi imedhamiria kuanzisha

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema, nchi za Magharibi zimedhamiria kudhoofisha hali ya ndani ya nchi hiyo na kuvuruga uthabiti wakati huu wa kukaribia kufanyika uchaguzi wa bunge la chini la Duma.

Sergei Lavrov amesema hayo leo alipohutubia semina iliyofanyika kwa anuani ya "Siasa za Nje za Russia: Mafanikio, Changamoto, Majukumu na Matarajio" na akabainisha kuwa: kwa kutekeleza mashinikizo ya kijeshi na kiuchumi dhidi ya majirani, Wamagharibi wanafanya juu chini ili kuanzisha "ukanda wa kuvuruga uthabiti" kandokando ya Russia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia vilevile ameashiria njama ya nchi za Magharibi ya kuvuruga uthabiti ndani ya nchi hiyo pia wakati wa kukaribia uchaguzi wa Duma na akasema: wananadharia wa kisiasa wa Magharibi wanajipinda kufanya kila wawezalo kuhusiana na suala hili; na kwa ajili ya kufikia lengo hilo hawachelei kutumia wenzo wowote ule usio wa insafu; wanatengeneza mambo yao wenyewe ya kubuni na kuzusha tuhuma zisizo na ushahidi wowote."

Uchaguzi wa bunge dogo la Russia la Duma umepangwa kufanyika tarehe 19 Septemba, ambapo wabunge 450 wa bunge hilo wanaohudumu kwa muda wa miaka mitano watachaguliwa.../

 

Tags