Jul 24, 2021 08:07 UTC
  • Rais wa Venezuela atangaza utayari wake wa kufanya mazungumzo na mrengo wa upinzani

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ametangaza kuwa, yuko tayari kushiriki katika mazungumzo na mrengo wa upinzani.

Rais Maduro amesema kuwa, yuko tayari kufanya safari nchini Mexico na kushiriki katika mazungumzo na wapinzani yaliyopangwa kufanyika nchini humo kwa minajili ya kuzipatia ufumbuzi hitilafu baina ya serikali yake na mrengo wa upinzani.

Duru mpya ya mazungumzo baina ya wawakilishi wa serikali na wapinzani imepangwa kufanyika mwezi ujao wa Agosti huko nchini Mexico lengo likiwa ni kuhitimisha mgogoro mkubwa wa kisiasa wa nchi hiyo iliyokjo kaskazini mwa Pwani ya  Amerika ya Kusini. Mazungumzo hayo yanayofanyika kwa upatanishi wa kimataifa yanapigiwa upatu na serikali ya Norway.

Ujumbe wa Norway unatarajiwa kufanya safari hivi karibuni humko nchini Venezuela kwa ajili ya kuuandaa mazingira na ajenda za mazungumzo hayo.

Juan Guaido, kiongozi wa upinzani nchini Venezuela

 

Kabla ya hapo, Rais Maduuro aliwahi kutangaza kuwa, ili kuondolewa nchi hiyo vikwazo vya Marekani yuko tayari kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Juan Guaido.

Katika miaka ya hivi karibuni Marekani imetumia njia ya mbalimbali kama wenzo wa vikwazo vikubwa vya kiuchumi na kisiasa, kuwasaidia wapinzani wa ndani na kuwapatia himaya na misaada ya kifedha na kisiasa hususan Juan Guaido, kiongozi wa upinzani na hata kumtambua kama Rais wa Venezuela ili kuiondoa madarakani serikali halali ya Maduro, lakini imefeli katika njama zake zote hizo.

Tags