Jul 25, 2021 08:04 UTC
  • Baraza la Usalama la UN kufanya kikao cha kuchunguza jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina

Mwakilishi wa kudumu wa Palestina katika Umoja wa Mataifa amesema, Baraza la Usalama la umoja huo litafanya kikao cha kuchunguza uvamizi na uchokozi unaofanywa na walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Riyadh al Mansour amesema, amemwandikia waraka Rais wa Baraza la Usalama, Katibu Mkuu na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutaka jamii ya kimataifa itekeleze jukumu lake kuhusiana na kadhia ya Palestina kwa kuchunguza uchokozi na uvamizi unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel na kuushinikiza utawala huo wa Kizayuni uheshimu sheria kuhusiana na ardhi za Palestina.

Al Mansour amebainisha kuwa, waraka huo aliotuma ni utangulizi kwa ajili ya kufanyika kikao hicho cha Baraza la Usalama siku ya Jumatano.

Imeripotiwa kuwa, tangu tarehe 3 Mei na baada ya walowezi wa Kizayuni kujenga mahema katika mlima wa Jabal Sabih na kuanza kujenga kitongoji cha Wazayuni katika eneo hilo, kitongoji cha Bita kilichoko kusini mwa mji wa Nablos huko Ufukwe wa Magharibi kinashuhudia mapigano ya kila leo baina ya wakazi wa kitongoji hicho na askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Katika upande mwingine wizara ya afya ya Palestina imetangaza kuwa askari wa Kizayuni wamemuua shahidi kwa kumpiga risasi Muhammad Munir At-Tamimi, kijana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 17 katika kijiji cha Nabiy Saleh.../