Jul 27, 2021 07:31 UTC
  • Waziri wa Ulinzi wa Marekani atiwa wasiwasi na wanajeshi wanaojiua

Waziri wa Ulinzi wa Marekani amesema ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka idadi ya wanajeshi wa nchi hiyo wanaojiua. Lloyd Austin amebainisha hayo alipokutana na wanajeshi wa Marekani huko Alaska.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani ameeleza kuwa, mashinikizo waliyonayo wanajeshi wao na kukataa kwao kupatiwa matibabu ya matatizo na magonjwa ya kiakili ni kati ya sababu kuu zinazopelekea kuongezeka visa vya kujiua miongoni mwa wanajeshi wa Marekani.  

Matatizo ya kiakli kati ya sababu za kujiua wanajeshi wa Marekani 

Austin ameongeza kuwa na hapa ninanukuu,"tunafahamu mashinikizo wanayokabiliana nayo wanajeshi wetu; na tuna wasiwasi sana na idadi ya wanajiua si tu hapa bali kwa wanajeshi wetu wote." Gazeti la US Today hivi karibuni liliripoti kuwa, wanajeshi wa Marekani wasiopungua 6 wamejiua huko Alaska. Baadhi ya ripoti pia zinasema kuwa ni wanajeshi 7 ndio waliojiua huko Alaska.  

Wanajeshi katika eneo hilo hukumbwa na fadhaa usingizi pale wanapkuwa katika hali ya hewa ya chini ya nyuzi 60 Celcius kutokana na baridi kali inayodumu kwa muda mrefu ikiambatana na giza na pale jua linapotoka hadi usiku wa manane. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la Marekani katika miaka ya karibuni limetumia zaidi ya dola milioni 200 ili kuboresha hali ya maisha ya wanajeshi wake. Mwaka 2018 wanajeshi wa Marekani wasiopungua 326 walijiua; na mwaka 2019 idadi hiyo iliongezeka hadi 350 na mwaka jana wa 2020 idadi ya wanajeshi wa Marekani waliojiua iliweka rekodi mpya baada ya wanajeshi 385 kujiua.