Jul 28, 2021 07:47 UTC
  • Russia yaitaka Marekani iwaondoe wanajeshi wake Iraq, Libya, Syria na Afghanistan

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameitaka Marekani iwaondoe wanajeshi wake huko Iraq, Libya, Afghanistan na Syria.

Maria Zakharova amewaambia waandishi wa habari mjini Moscow kwamba Marekani inapaswa kuwaondoa wanajeshi wake wote katika nchi za Syria, Afghanistan, Libya na Iraq. Zakharova alikuwa akijibu matamshi yaliyotolewa na Naibu Mkuu wa Vikosi vya Majeshi ya Marekai John Hayton aliyedai kuwa, Washington itabakisha idadi ndogo ya wanajeshi huko Iraq, Syria, Afghanistan na Libya kwa ajili ya kukabiliana na eti na makundi ya kigaidi na vitisho vya China na Russia.

Marekani iliivamia ardhi ya Afghanistan Oktoba mwaka 2001 kwa kisingizio cha kushambuliwa minara pacha ya jengo la Biashara la Kimataifa mjini New York kwa shabaha eti ya kukabiliana na ugaidi na kuliondoa madarakani kundi la Taliban. Hata hivyo baada ya kuikalia kwa mabavu nchi hiyo kwa kipindi cha mika 20 imelazimika kukimbia Afghanistan na kuiacha nchi hiyo katika hali mbaya ya kiusalama na ukosefu wa amani. 

Wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Afghanistan 

Mwaka 203 pia Marekani na washirika wake waliishambulia Iraq kwa kisingizio cha kuwepo silaha za maangamizi ya umati nchini humo, hatua ambayo haikuwa na faida ghairi ya kusababisha uharibifu usio na kifani ikiwa ni pamoja na kuharibu miundombinu, kuua maelfu ya raia wa Iraq, kuimarisha makundi ya kigaidi na kuzusha migogoro isiyoisha ya kisisa nchini humo.

Washington pia inaendelea kupora utajiri wa Syria kwa kutumia majeshi yake yaliyovamia na kukalia sehemu ya ardhi ya nchi hiyo ambayo inatumiwa na Marekani kutoa mafunzo kwa makundi ya kigaidi na waasi wanaopigana kwa shabaha ya kuiondoa madarakai serikali halali na iliyochauliwa na wananchi wa Syria. 

Tags