Jul 28, 2021 13:48 UTC
  • Watu zaidi ya milioni 50 wapata corona barani Ulaya

Watu zaidi ya milioni 50 wameambukizwa kirusi cha corona barani Ulaya.

Takwimu za mtandao wa worldometers zinaonyesha kuwa, hadi sasa watu zaidi ya milioni 50 na 869,000 wamepata maambukizi ya corona barani Ulaya ikilinganishwa na takwimu jumla za kimataifa za maambukizi ya virusi hivyo zilizotolewa kuanzia mwezi Disemba mwaka 2019 hadi Julai 27 mwaka huu.  

Hadi kufikia sasa watu zaidi ya watu milioni moja na 127,000 wameaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 katika nchi za Ulaya. Russia, Ufaransa, Uingereza, Uhispania, Italia na Ujerumani kwa utaratibu zimesajili idadi kubwa ya maambukizi ya corona. Nchi hizo sita zinaongoza kwa kuwa na zaidi kubwa zaidi ya walioambukizwa ugonjwa wa Covid-19 barani Ulaya.   

Huko Marekani pia maambukizi ya virusi vya corona aina ya Delta yamepelekea kuongezeka pakubwa idadi ya wagonjwa na wahanga wa ugonjwa wa Covid-19 nchini humo.

Ongezeko la maambukizi ya corona Marekani  

Televisheni ya CNN imeripoti kuwa, maambukizi ya corona nchini Marekani yameongezeka kwa asilimia 60, na kwamba kila siku kwa wastani watu elfu 49 wanaambukizwa virusi ugonjwa wa Cpvid-19 nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vifo vya corona pia vimeongezeka kwa asilimia 8 huko Marekani katika siku saba zilizopita na idadi ya vifo inatajwa kufikia watu 272 kwa siku.