Jul 29, 2021 08:02 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Asilimia 60 ya wananchi wa Marekani wanamlaumu Biden kwa mfumuko wa bei

Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa huko Marekani unaonyesha kuwa, asilimia 60 ya wananchi nchini humo wanaamini kuwa Rais wa nchi hiyo Joe Biden ndiye anayepaswa kulaumiwa kwa mfumuko wa bei ambao haujawahi kushuhudiwa nchini humo katika miaka 13 ya karibuni.

Matokeo ya uchunguzi huo mpya wa maoni uliofanywa kwa pamoja na Jarida la Political na Taasisi ya Morning Consult yanaonyesha kuwa, asilimia 60 ya wananchi wa Marekani wanaamini kuwa sera za serikali ya Rais Joe Biden ni sababu kuu ya kuongezeka mfumuko huo mkubwa wa bei nchini; huku asilimia 28 tu ya watu wakisema Biden hausiki na mfumuko huo mkubwa. 

Wakati huo huo matokeo ya uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa na Taasisi ya Gallop na kuchapishwa Ijumaa iliyopita unaonyesha kuwa, uungaji mkono wa wananchi kwa Rais Biden umepungua kwa asilimia sita na kufika asilimia 50 sasa ikilinganishwa na mwezi Juni mwaka huu.

Ughali wa kupindukia wa bidhaa za msingi nchini Marekani

Kupungua uungaji mkono wa wananchi kwa Rais Joe Biden ni matokeo ya wasiwasi mkubwa walionao wananchi kuhusu kuongezeka pakubwa kwa mfumuko wa bei nchini, kuongezeka maambukizi ya corona na mwenendo wa kusuasua wa mchakato wa utoaji chanjo dhidi ya ugonjwa  UVIKO-19 huko Marekani.  

Mfumuko wa bei nchini Marekani umeshtadi pakubwa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 13 ya hivi karibuni ikiwa imepita karibu miezi saba tu tangu kuingia madarakani serikali ya Rais Joe Biden. 

Tags