Aug 09, 2021 07:41 UTC
  • Amnesty yaunga mkono kampeni ya kususiwa utawala wa kibaguzi wa Israel

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeunga mkono hatua ya kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza malai (ice cream) na mtindi ya Marekani ya kuususia utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amnesty International imetangaza kuwa, uamuzi uliochukuliwa na kampuni ya Ben & Jerry's ambayo ndiyo kubwa zaidi inayozalisha mtindi na malai (ice cream) nchini Marekani ya kusitisha uuzalisaji wa bidhaa zake kwa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vya utawala wa Israel ni halali, ya dharura na inayokidhi sheria za kimataifa.

Taarifa ya Amnesty International imeongeza kuwa, msimo wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina ni zaidi ya kukiuka sheria za kimataifa, kwani mbali na kwamba ujenzi huo ni kinyume cha sheria, vilevile unakiuka na kukanyaga haki za binadamu za raia wa Palestina.

Vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, Palestina

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema, kustawishwa uchumi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kunashajiisha ujenzi wa vitongoji hivyo na kwamba makampuni yanayosaidia kustawisha maeneo hayo pia yatakuwa washirika katika jinai zinazofanywa dhidi ya Wapalestina. 

Siku chache zilizopita kampuni ya Ben & Jerry's ya Marekani ilitoa taarifa ikitangaza kuwa, uuzaji wa bidhaa zake kwa vitongoji vya walowezi wa kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu unakwenda kinyume na maadili ya kampuni hiyo na kwa sababu imechukua hatua ya kusimamisha suala hilo. 

Tags