Aug 15, 2021 02:24 UTC
  • Poland yakataa kulipa fidia kwa Marekani na Israel

Waziri Mkuu wa Poland, Mateusz Morawiecki amepinga ukosoaji uliolenga hatua ya Bunge la nchi hiyo ya kupasisha sheria mbili zinazohusiana na umiliki wa vyombo vya habari na Holocaust na kusema kuwa, hakuna uwezekano wa kuruhusu utawala wa Kizayuni wa Israel kumiliki vyombo vya habari vya Poland.

Awali Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Antony Blinken alikuwa ameeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hatua ya Bunge la Poland ya kupasisha sheria inayozuia kurejeshwa mali za familia za wahanga wa kile kinachodaiwa kuwa ni mauaji ya Holocaust ambayo pia inayokwamisha kazi za kituo cha habari kilichoanzishwa kwa uwekezaji wa Marekani huko Poland. 

Sheria ya vyombo vya habari iliyopasishwa siku ya Jumatano iliyopita katika Bunge la Poland inazuia makampuni ya nje ya eneo la kiuchumi la Ulaya kumiliki au kuwa na hisa kuu katika vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo. Upande unaopata hasara kubwa zaidi kutokana na sheria hiyo ni kampuni moja ya Kimarekani. Kundi la vyombo vya habari la Discovery Inc ndilo linalomiliki hisa kubwa zaidi ya kanali ya TVN ambayo ndiye yenye watazamaji wengi zaidi nchini Poland, na chombo kinachoikosoa zaidi serikali ya Waziri Mkuu wa mrengo wa kulia wa nchi hiyo, Mateusz Morawiecki. 

Kupasishwa sheria hiyo mpya ya vyombo vya habari ambayo pia inabidi iidhinishwe na Seneti ya Poland, kunaweka vizuizi vingi mbele ya makampuni yasiyo ya Ulaya kama ya Marekani na Israel, yanayotaka kumili vyombo vya habari nchini Poland. 

Mbali na kupinga suala la kukabidhi umiliki wa baadhi ya mali zilizoko nchini humo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel vikiwemo vituo kadhaa vya habari, Waziri Mkuu wa Poland amesisitzia kuwa: "Tunataka kuwa na mazingira yatakayozuia makampuni kutoka nje ya Ulaya (akiashiria makampuni ya Israel) kuweza kununua vyombo vya habari nchini Poland."

Mateusz Morawiecki

Uhusiano wa Warsaw na Washington umekumbwa na changamoto nyingi tangu Joe Biden aliposhika madaraka ya nchi huko Marekani kutokana na hitilafu za pande mbili juu ya masuala kama madai ya kuwa hatarini mfumo wa demokrasia nchini Poland, haki za maingiliano ya kingono baina ya watu wenye jinsia moja, uwekezaji wa kigeni na jinsi ya kuamiliana na manusura wa kile kinachoitwa mauaji ya Holocaust. Sheria hii mpya ya vyombo vya habari inazidisha na kupanua zaidi hitilafu za pande hizo mbili.

Sambamba na kupasisha sheria mpya ya vyombo vya habari, Bunge la Poland pia limepasisha sheria nyingine inayotatiza suala la kurejeshwa mali zilizotwaliwa na Manazi wakati wa Vita vya Pili Pili vya Dunia kwa wanaodaiwa kuwa manusura wa Holocaust. Marekani na Israel zilikuwa zimetoa wito wa kuzuia kupasishwa sheria hiyo.

Hadi sasa Israel imepokea kiwango kikubwa sana cha fidia kutoka kwa nchi za Ulaya kwa kutumia kisingizio cha eti mauaji ya Holocaust na nafasi ya nchi hizo katika suala hilo. Ujerumani ambayo ndiyo mtuhumiwa mkuu wa Holocaust, tayari imeipatia Israel mabilioni ya yuro kwa kisingizio hicho.

Poland ambayo ni moja kati ya nchi zinazotajwa kuwa na kambi zilizotumiwa na Manazi wa Ujerumani, imekanusha tuhuma za kuhusika katika mauaji yanayodaiwa kufanywa dhidi ya Wayahudi na kupinga waziwazi mwenendo wa unyang'anyi na utumiaji mabavu wa kuupatia fidia utawala wa Kizayuni wa Israel na kuhalalisha suala la kufunguliwa kesi mahakamani kuhusu kadhia hiyo.

Serikali ya Poland imetangaza kuwa haihusiki kwa vyovyote vile na Holocaust. Suala hilo limeukasirisha utawala wa Kizayuni wa Israel ambao umefanya jitihada kubwa za kuituhumu Poland kuwa inawachukia Wayahudi! Msimamo imara wa Poland katika kadhia hii unawazuia Wazayuni kufikia malengo yao ya kupata fedha na milki zinazodaiwa kuwa ni za wahanga wa Holocaust.          

Tags