Sep 02, 2021 02:59 UTC
  • Magaidi wajisalimisha kwa jeshi la Syria katika eneo la Dar'a

Duru za habari zimetangaza kuwa, kundi la watu wenye silaha la eneo la Dar'a wa kusini mwa Syria limejisalimisha kwa jeshi la nchi hiyo na Kiarabu na kukabidhi silaha zao.

Shirika rasmi la habari la Syria limetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, mchakato wa kufikiwa mapatano baina ya serikali ya Syria na makundi yenye silaha huko Dar'a umeanza rasmi.

Taarifa hiyo imesema kuwa, vituo kadhaa vimewekwa katika eneo la Dar'a kwa ajili ya kufuatilia upatanishi na mapatano baina ya watu wenye silaha na jeshi la serikali. Aidha kumetengwa eneo maalumu la "al Arbain" ambalo linatumika kwa ajili ya kukusanywa silaha za wapiganaji hao.

Duru za kuaminika zinasema kuwa, makundi yenye silaha ambayo hayakubaliani na vipengee vya usimamishaji vita, yatalazimika kuondoka katika eneo la Dar'a al Balad na kwenda al Mukhayyam.

Mwanajeshi wa Syria akipandisha bendera ya taifa

 

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya jeshi la Syria kuyapa muda maalumu makundi yenye silaha ya imma kujisalimisha au kuondoka katika eneo hilo baada ya kufeli mazungumzo ya kuacha jeshi la Syria kuyazingira maeneo walipojificha watu hao wenye silaha. Eneo hilo lilikuwa linatumika kwa ajili ya kufanya mashambulio ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dar'a.

Magenge hayo yaliliomba jeshi la Syria lisimamishe vita ili yaweze kujisalimisha, lakini mazungumzo ya kufanyika zoezi hilo yamefelishwa na mivutano ndani ya magenge hayo ambayo mengine hayako tayari kuheshimu vipengee vya makubaliano ya kusimamisha vita. 

Tags