Sep 08, 2021 08:55 UTC
  • Scotland kuanzisha tena mkakati wa kujitenga na Uingereza

Waziri wa Kwanza wa Scotland amesema kuwa ana nia ya kuitisha kura ya maonii ya kujitenga na Uingereza hadi kufikia mwaka 2023.

Nicola Sturgeon amesema kuwa suala la kujitenga na Uingereza ni miongoni mwa ajenda za serikali yake na kwamba mwaka huu Bunge la Scotland halitajadili muswada wa kuitisha kura ya maoni.

Waziri wa Kwanza wa Scotland amesema, kura ya maoni ya kujitenga na Uingereza itaitishwa baada ya kumalizika mgogoro wa virusi vya corona. 

Kabla ya kuibuka virusi vya corona nchini Scotland, Bunge la nchi hiyo Januari mwaka 2020 lilipasisha muswada wa kuitishwa kura ya pili ya maoni kujitenga na Uingereza. Wakati huo Nicola Sturgeon alitoa wito wa kuitishwa kura hiyo ya maoni lakini ombi hilo lilikataliwa na Wazirii Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson. 

Nicola Sturgeon

Kura ya kwanza ya maoni ya kujitenga Scotland na Ungereza iilifanyika mwaka 2014; miaka miwili tu kabla ya kura ya maoni ya kihistora ya kujitenga Uingereza na Umoja wa Ulaya (Brexit).

Hatua ya Uingereza ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya ambayo ilipingwa na wakazi wa Scotland imechochea zaidi hamu ya Waskochi ya kujitenga na Uingereza.  

Tags