Sep 14, 2021 15:01 UTC
  • Maria Zakharova
    Maria Zakharova

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa lengo la mpango wa Marekani eti wa kuimarisha demokrasia nchi ya Ukraine ni kuiweka chini ya mashinikizo Russia na kuyumbisha hali ya mambo katika eneo hilo.

Maria Zakharova amesema kuwa mpango huo wa Marekani wa eti  kuifanya Ukraine nchi ya kidemokrasia na kuifadhili kifedha hauna maslahi kwa wananchi wa Ukraine bali umekusudia kuiwekea mashinikizo Russia.  

Hali ya mvutano na mzozo iligubika uhusiano wa nchi mbili za UKraine na Russia baada ya matukio ya mwaka 2014 na kura ya maoni ya kukiunganisha kisiwa cha Crimea na Russia, na vilevile baada ya mapigano yaliyotokea kati ya jeshi la Ukraine na raia wa nchi hiyo wenye asili ya Russia wanaounga mkono mpango wa kujitenga maeneo ya mashariki na Ukraine .  

Kisiwa cha Crimea 

Uhusiano wa Magharibi na Moscow pia umeharibika kuanzia mwaka 2014 juu ya mambo manne makuu ya kupanua ushawishi wa kijeshi ya Jumuiya ya Kijeshi ya Nchi za Magharibi (NATO) na hususan Marekani karibu na katika mipaka ya Russia huko Ulaya mashariki, kuhusu mgororo wa Ukraine, Bahari ya Baltic na mgogoro wa Syria. 

Marekani na Umoja wa Ulaya zimeiwekea Russia vikwazo vya kiuchumi na kifedha tangu mwaka 2014; hatua iliyokosolewa na kupingwa na Moscow. 

Tags