Sep 16, 2021 02:24 UTC
  • Russia: Hakuna ushahidi wowote kuwa Iran inafanya jitihada za kuunda silaha ya nyuklia

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika jumuiya za kimataiifa amesema kuwa, hadi sasa Iran haijaonesha kuwa, inafanya mikakati ya kuunda silaha za nyuklia na kwamba tuhuma zinazotolewa katika uwanja huo zina lengo la kuvuruga mazungumzo ya Vienna.

Mikhail Ulyanov amesema kuwa, uundaji wa bomu la nyuklia kwa nchi yoyote isiyo na silaha za nyuklia ni jambo gumu mno. Amesisitiza kuwa hakuna alama au ushahidi wowote unaoonesha kuwa, Iran inafanya mikakati ya kuwa silaha hizo. 

Mwanadiplomasia huyo wa Russia amesisitiza kuwa, Moscow inakaribisha tangazo lililotolewa na Iran kwamba, iko tayari kushiriki tena katika mazungumzo ya kuhuisha makubaliano ya nyukla ya JCPOA. 

Mikhail Ulyanov Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika jumuiya za kimataiifa amesema kuwa, tarehe ya kuanza tena mazungumzo hayo bado haijaainishwa lakini msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, mataanza hivi kariibuni.  

 

Tarehe 8 Mei 2018 rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump alichukua hatua ya upande mmoja na ya kinyume cha sheria ya kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuanza kutekeleza sera aliyoiita "mashinikizo ya juu kabisa" dhidi ya Iran.

Maafisa wa serikali ya sasa Marekani inayoongozwa na Joe Biden wamekiri kadhaa kuwa sera hiyo ya Trump imegonga mwamba na kudai kwamba wanataka kuirejesha Washington kwenye JCPOA; lakini hadi sasa wanakaidi kutekeleza hatua zinazohitajika ili kuweza kurejea katika makubaliano hayo.