Sep 16, 2021 12:02 UTC
  • UN yakiri kuwa haina uwezo wa kutatua mgogoro wa Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, pembenekezo lolote la kudai kuwa umoja huo unaweza kutatua matatizo ya Afghanistan ni ndoto tu ambazo haziwezi kuaguka.

António Guterres amesema hayo akiashiria nguvukazi ya binadamu na gharama kubwa zilizotumiwa na Marekani na waitifaki wake wa Ulaya katika kipindi cha miaka 20 iliyopita huko Afghanistan na kusema kuwa, kwa kuzingatia kwamba madola hayo yameshindwa kutatua migogoro ya Afghanistan licha ya kutumia fedha nyingi na roho za watu wengi pamoja na muda mrefu wa miongo miwili, litakuwa ni jambo lisilo sahihi kufikiri kwamba Umoja wa Mataifa unaweza kutatua matatizo ya nchi hiyo hata ikipewa muda wa miongo mingi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema hayo kabla ya kongamano la kila mwaka la umoja huo ambalo limepangwa kufanyika wiki ijayo mjini New York Marekani. Amesisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa unaunga mkono juhudi za kuilazimisha Taliban iunde serikali pana na kubwa itakayoshirikisha watu wa matabaka yote.

Wakimbizi wa Afghanistan

 

Siku chache zilizopita pia, António Guterres alisema kuwa jamii ya kimataifa ina deni kubwa kwa wananchi wa Afghanistan na kwamba suala muhimu si kile ambacho watapatiwa wananchi wa taifa hilo bali ni deni la jamii ya kimataifa kwa wananchi wao.

Guterres alisema hayo, alipohutubia mkutano juu ya mustakabali wa hali ya kibinadamu ya Afghanistan uliofanyika kwa njia ya mtandao na kuhudhuriwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kama lile la kuhudumia watoto UNICEF na la misaada ya kibinadamu, OCHA.

Tags