Sep 17, 2021 07:54 UTC
  • China yalaani muungano mpya wa kijeshi wa pande tatu za Marekani, Uingereza na Australia

China imelaani ushirika mpya wa usalama wa kihistoria kati ya Marekani, Uingereza na Australia. Serikali ya Beijing imesema muungano huo una kile ilichokitaja kama maono yasiyofaa.

Makubaliano hayo yatazifanya Marekani na Uingereza kuipatia Australia teknolojia ya kuunda kwa mara ya kwanza manowari zenye uwezo wa kinyuklia.

Kuanzishwa kwa muungano huo kunaonekana kama juhudi za kuukabili ushawishi wa China katika eneo linalozozaniwa la kusini mwa China.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umesema haukuarifishwa kuhusu kuundwa kwa ushirika mpya wa kijeshi kati ya Marekani, Uingereza na Australia.

Hali ya kijeshi katika bahari ya kusini mwa China

Hayo ni  kwa mujibu wa msemaji wa Kamisheni Kuu ya Umoja wa Ulaya Peter Stano, ambaye ameongeza kwamba watajaribu kuzungumza na Marekani, Uingereza na Australia ili kujua kinachoendelea.

Stano amebainisha kuwa nchi za Ulaya zitajadiliana kuhusu athari ya uamuzi wa nchi hizo tatu.

Viongozi wa Marekani, Uingereza na Australia wameutangaza ushirika huo mpya ili kuzuia kile kinachodaiwa kama ushawishi wa China unaozidi kupanuka katika ukanda wa Indo-Pasifiki.../

Tags