Sep 19, 2021 02:24 UTC
  • Jeshi la China lafanya mazoezi ya kijeshi katika langobahari la Taiwan

Sambamba na kuwepo kijeshi manowari za Marekani katika maji ya China, jeshi la China limetangaza kuwa vikosi vyake vinafanya mazoezi ya kijeshi katika langobahari la Taiwan.

Shi Yi, msemaji wa kamandi ya mashariki ya jeshi la China ametangaza kuwa, vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vimefanya maneva ya angani na baharini katika langobahari la Taiwan kufuatia kupita manowari ya Marekani katika eneo hilo.

Kabla ya hapo, wizara ya ulinzi ya China ilitoa taarifa kulalamikia kitendo cha manowari ya jeshi la wanamaji la Marekani aina ya  USS KIDD na meli moja ya gadi ya pwani ya nchi hiyo kupita katika langobahari la Taiwan.

Manowari za Marekani katika maji ya China

Wizara ya ulinzi ya China imesema, hatua hiyo ya Marekani ni ya kichochezi na ikatangaza kuwa, Washington ndio tishio kubwa zaidi kwa amani na uthabiti katika langobahari la Taiwan.

Serikali ya Beijing imesisitiza mara kadhaa kuhusu ulazima wa kuheshimiwa msingi wa uwepo wa China moja iliyoungana inayojumuisha ardhi ya Taiwan.../