Sep 20, 2021 08:01 UTC
  • Kongresi kuzuia mauzo ya silaha kwa tawala za Saudi Arabia na Israel

Mbunge wa Kongresi ya Marekani amebuni muswada unaopiga marufuku uuzaji wa silaha za nchi hiyo kwa tawala za Saudi Arabia na Israel.

Alexandria Ocasio-Cortez ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba amefanya mabadiliko katika muswada wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022 ambayo yanapiga marufuku uuzaji wa baadhi ya silaha kwa Saudi Arabia kwa sababu ya faili la mauaji yaliyofanywa na utawala huo dhidi ya mwandishi habari na mkosoaji wa utawala huo, Jamal Khashoggi na vile marufuku ya kuuza silaha hizo kwa utawala wa Israel kwa kushambulia jesngo la vyombo vya habari katika Ukanda wa Gaza.

Jamal Khashoggi, aliuawa na kukatwa vipande vipande kwa amri ya mrithi wa ufalme wa Saudia, Muhammad bin Salman

Marekebisho hayo pia yanazuia kuzwa baadhi ya silaha kwa serikali ya Colombia kwa sababu ya kuwakandamiza waandamanaji.

Iwapo yatapasihwa, marekebisho hayo yatazuia kuuzwa silaha makini kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwemo shehena ya silaha za JDMA yenye thamani ya dola milioni 735.

Muswada huo umemkasirisha sana balozi wa Israel nchini Marekani na vilevile balozi na mwakilishi wa utawala huo katika Umoja wa Mataifa

Tags