Sep 22, 2021 12:31 UTC
  • Theluthi moja ya watu wazima wa mji wa Houston Marekani hawajui kusoma na kuandika

Imeelezwa kuwa theluthi moja ya watu wazima katika mji wa Houston, ambao ni mji wa nne wenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini Marekani hawajui kusoma na kuandika.

Kwa mujibu wa chaneli ya televisheni ya ABC, Houston, ambao ni mji wenye idadi kubwa zaidi ya watu katika jimbo ka Texas una jumla ya watu milioni mbili na laki tatu.

Wataalamu wanasema, moja ya sababu ya mji huo kuwa na watu wengi wasiojua kusoma na kuandika ni wazazi wenyewe ambao kutokana na kukosa maarifa hayo ya msingi hawawezi kuwasaidia watoto wao katika masomo yao ili waweze kufaulu.

Sababu nyingine iliyotajwa kuwa inachangia hali hiyo ya kusikitisha ni kutokuwepo mfumo mzuri na sahihi wa elimu ya msingi na kukosa fursa ya kupata elimu akthari ya watu wa matabaka ya kati na chini katika jamii, hususan wasio Wazungu.

Utoaji elimu ya msingi ya kujua kusoma na kuandika kwa watu wazima Houston, Marekani

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya televisheni ya ABC, watoto wanaocheleweshwa kwa mwaka mmoja kupelekwa skuli za elimu ya msingi hubaki nyuma sana kimasomo na kiufahamu kulinganisha na wenzao wa rika na umri mmoja, na jambo hilo huwafanya waanze kidogo kidogo kupoteza matumaini. Isitoshe, hakuna mtu anayeshughulishwa na suala la elimu na mustakabali wa watoto wasio wazungu hususan wa familia maskini nchini Marekani.

Raia mmoja aisyejua kusoma na kuandika katika mji wa Houston ameeleza katika mahojiano na chaneli ya televisheni ya ABC kwamba, alihukumiwa kifungo cha miezi miwili jela kwa sababu tu ya kutojua kusoma na kuandika, baada kuungama kosa kimakosa kwa kusaini waraka wa mahakama bila kufahamu maana na madhumuni ya maelezo ya kisheria yaliyoandikwa na hakimu.

Raia huyo amefafanua kuhusu mkasa huo kwa kusema: "hakimu wa mahakama aliniuliza jambo moja mara kadhaa; na wakati nilipomueleza kwamba, sifahamu madhumuni uliyokusudia alinambia, kama unataka urudi nyumbani saini chini ya waraka huu. Na mimi nikausaini waraka huo bila kutambua kuwa nitahukumiwa kwenda jela.../