Sep 26, 2021 04:33 UTC
  • Pew: Rais Joe Biden wa Marekani ana aina fulani ya

Asilimia kubwa ya washiriki katika uchunguzi wa maoni uliofanywa na Taasisi ya Pew wanasema kwamba Rais wa Marekani, Joe Biden ana aina fulani ya "ujinga".

Jarida la Washington Examiner limeripoti kuwa, inaonekana kipindi cha urais wa Joe Biden hakiendi kirahisi kama ilivyotarajiwa na kwamba ni asilimia 43 tu ya washiriki katika uchunguzi huo wa maoni ndio wanaoamini kuwa Biden yuko sawa kiakili. 

Ripoti hiyo imesema kuwa, mbali na mgogoro wa mipaka, mivutano iliyopo baina ya Wademocrati ndani ya Kongresi, kuwepo maafisa wasiofaa wa fya ambao hawakuweza kusimamia vyema tatizo la maambukizi ya corona na kuondoka kwa kukurupuka majeshi ya Marekani huko Afghanistan ni miongoni mwa sababu zinazowafanya Wamarekani wengi waamini kuwa rais wao sio mtu hodari na mwenye akili.

Asilimia 56 ya walioshiriki katika uchunguzi wa maoni wa Pew wamesema kuwa, si sawa tena kumtaja Joe Biden kuwa ni mtu "mwenye akili".

Taarifa ya Pew pia imesema kuwa, ikilinganishwa na mwezi Machi mwaka huu pia, idadi ndogo ya watu wazima wa Marekkani wanasema kuwa, Biden anawajali. 

Katika miezi ya hivi karibuni kiongozi huyo wa Marekani amekumbwa na ukosoaji mkubwa wa vyombo vya habari na duru za wanasiasa wanaomlaumu kwa kukosa busara na uongozi wake dhaifu katika masuala mengi ya ndani ya nje ya nchi hususa baada ya uamuzi wake wa kuliondoa bila mpangilio jeshi la nchi hiyo huko Afghanistan.