Sep 27, 2021 11:33 UTC
  • Joe Biden
    Joe Biden

Mtandao wenye mfungamano na Kongresi ya Marekani umekosoa utendaji wa rais wa nchi hiyo ndani na nje ya nchi na kuripoti kuwa, Joe Biden ameifanya dunia kuwa mahali hatari sana.

Ripoti ya mtandao wa The Hill imeashiria hotuba iliyotolewa na Joe Biden katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuripoti kuwa: Wiki iliyopita Biden alitoa hotuba yake ya kwanza katika Baraza Kuu la UN na kudai tena kwamba, "Marekani imerudi" na kwamba nchi hiyo inakusudia kuwa mstari wa mbele na kushika usukani katika changamoto zote kubwa za kipindi cha sasa. Mtandao huo umesama, Marekani inapaswa kuwa kama alivyosema Biden, lakini inasikitisha kwamba ukweli wa mambo ni kinyume chake. 

Sehemu moja ya ripoti ya The Hill imeashiria hatua ya Marekani kuondoa majeshi yake huko Afghanistan kwa papara na bila ya mpangilio na kuandika kuwa: Biden si tu kwamba hakuweza kufanya lolote kwa ajili ya Marekani, lakini pia anaifanya dunia kuwa eneo hatari zaidi. 

Majeshi ya Marekani yakikimbi Afghanistan

Kuhusu suala la waitifaki wa Marekani kukosa imani na nchi hiyo, The Hill limeandika kuwa, waitifaki wakubwa wa Marekani hawana tena imani na Biden kama mshirika muhimu, na wananchi wa Marekani hawaamini kuwa Biden anaweza kulinda na kudhamini malengo yao ya kimsingi. 

Serikali ya Rais Joe Biden inakabiliwa na changamoto nyingi kubwa ikiwa ni pamoja na mgogoro wa maambukizi ya corona aina ya Delta, upinzani wa chanjo ya kulazishwa kwa wafanyakazi wa umma, wimbi la wahajiri kutoka Haiti katika mpaka wa Texas na athari mbaya za kuondoka bila ya mpangilio wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.