Oct 08, 2021 02:50 UTC
  • Russia: Matatizo ya bara la Afrika inapasa yatatuliwe na viongozi wa nchi za Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema, matatizo ya baraza la Afrika inapasa yatatuliwe na viongozi wa nchi za Afrika na akaongeza kwamba Russia inaweza kuandaa mazingira ya kuwekwa askari wa kulinda amani barani humo.

Sergey Lavrov ameyaema hayo mjini Moscow katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya pamoja na mwenzake wa Rwanda Vincent Biruta.

Ameashiria msimamo wa Russia wa kufungamana na ahadi na msimamo wake wa kudumisha uthabiti katika bara la Afrika na akasema, Moscow itafungua njia kwa ajili ya kufanyika kikao baina ya viongozi wa nchi za Kiafrika na Rais Vladimir Putin wa Russia.

Sergey Lavrov na Vincent Biruta wakiamkiana walipokutana mjini Moscow

Katika mkutano huo wa pamoja na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta amesema, Russia ni mshirika imara wa nchi yake katika nyanja tofauti ikiwemo ya nishati na akaongeza kuwa Kigali inafanya juhudi za kuhakikisha yanafikiwa makubaliano baina yake na Moscow yatakayokuwa na manufaa kwa watu wa nchi hizo mbili.../

Tags