Oct 09, 2021 03:28 UTC
  • Russia and China: Shughuli za kibaolojia za Marekani zimeuweka hatarini usalama wa dunia

Russia na China zimetoa taarifa ya pamoja zikikosoa shughuli za vituo vya kibaolojia vya Marekani na kusema vinauweka hatarini usalama wa dunia.

Taarifa ya pamoja ya China na Russia imeeleza kuwa, shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na zaidi ya vituo 200 vya baolojia vya Marekani na waitifaki wake katika maeneo mbalimbali duniani zimeibua wasiwasi kimataifa na hatua hiyo inakiuka mkataba unaopiga marufuku silaha za kibaolojia. 

Silaha za kibaolojia za Marekani 

Taarifa ya pamoja ya Russia na China imesisitiza kuwa, shughuli za vituo hivyo vya baolojia vya Marekani na waitifaki wake ni tishio kubwa kwa usalama wa taifa la Russia na China na zinatoa pigo kwa usalama wa kieneo.  

China na Russia zimesema kuwa zinafungamana na mkataba unaopiga marufuku uundaji na ulimbikizaji wa silaha za kibaolojia na zenye sumu na kusisitiza azma yao ya kulinda hadhi na malengo ya mkataba huo. 

Katika mlolongo wa malengo yake yasiyo ya kibinadamu Marekani imeanzisha maabara za kibaolojia katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo huko Ukraine, Kazakhstan, Uzbekistan, Georgia, Armenia, Korea Kusini, Colombia, Indonesia na barani Afrika.   

Tags