Oct 13, 2021 07:39 UTC
  • Taliban yazionya Marekani na nchi za Ulaya dhidi ya kuidhoofisha serikali yake

Msimamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan amezitahadharisha tawala za Magharibi juu ya hatua yoyote ya kuudhoofisha utawala mpya ulioundwa na kundi hilo.

Amir Khan Muttaqi ametoa indhari hiyo katika mkutano na wawakilishi wa Marekani na nchi za Ulaya uliofanyika katika mji mkuu wa Qatar, Doha na kueleza kwamba, kuidhoofisha serikali mpya ya Afghanistan iliyoundwa na Taliban kutaiathiri moja kwa moja dunia katika sekta za usalama, uchumi na uhajiri.

Muttaqi amezihutubu nchi za Magharibi akisema, "kutumia mbinu na taktiki ya mashinikizo hakujawa na tija yoyote, kwa hivyo acheni tuchague njia ya maelewano na mashirikinao ya ujengaji."

Amir Khan Muttaqi

Kundi la Taliban, ambalo lilitwaa madaraka nchini Afghanistan mwezi Agosti mwaka huu sambamba na kuondoka askari wa Marekani katika nchi hiyo baada ya vita vya miaka 20, linapigania kutambuliwa rasmi na nchi za dunia serikali ya muda liliyounda; ili kufuatia hatua hiyo liweze kupatiwa misaada ya kuinusuru nchi hiyo na maafa ya kibinadamu na kupunguza athari za hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili.../

Tags