Oct 14, 2021 02:21 UTC
  • Vladmir Putin
    Vladmir Putin

Rais Vladmir Putin wa Russia amesema kuwa kiwango cha chini ya mapato ya aghalabu ya wananchi wa Russia ndio adui mkuu wa nchi hiyo na kueleza kuwa adui mkubwa zaidi wa Warussia ni mapatano ya kiwango cha chini ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo.

Rais Putin amesema hayo alipokutana na wawakilishi wa Bunge jipya la la Russia (Duma) na kuongeza kuwa, Russia na watu wake wote wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazofanana lakini adui mkuu wa nchi hii na tishio la usalama na ustawi wa Russia ni kiwango cha chini cha mapatano ya raia. 

Umaskini adui mkuu wa Russia 

Rais wa Russia amesisitiza umuhimu wa serikali kuzisaidia familia  nchini humo na kueleza kuwa, katika miaka ijayo serikali inapasa kuandaa mfumo wa kuzisaidia familia kuanzia kipindi cha akina mama wanapokuwa waja wazito hadi watoto wao wanakapomaliza shule. 

Rais Vladmir Putin amesema juhudi zinapasa kufanywa ili kuwazidishia wananchi mapato yao, kuandaa fursa za ajira mpya katika maeneo yote ya nchi, kuandaa uwanja mzuri wa ustawi wa kiuchumi na  kuzisaidia sekta zinazohitaji teknolojia ya kisasa. 

Tags