Oct 17, 2021 02:27 UTC
  • Wataalamu watahadharisha kuhusu hatari ya kirusi cha Nipah

Wataalamu wa masuala ya virusi wametahadharisha kuhusu athari mbaya za maambukizi ya kirusi cha Nipah kwa watu duniani hususan katika kipindi hiki ambapo dunia inashughulishwa na mapambano dhidi ya kirusi hatari cha corona.

Prof Dame Sarah Gilbert, mwanasayansi aliyebuni chanjo ya corona ya Oxford-AstraZeneca ametahadharisha kwamba, kuna uwezekano kirusi cha Nipah kikasababisha maambukizi ya kuangamiza wanadamu baada ya Covid-19 katika kipindi hiki ambapo dunia imejikita katika mapambano dhidi ya corona.

Virusi vya Nipah huambukizwa kwa wanadamu kupitia wanyama. Mlipuko wa kwanza unaojulikana ulitokea Malaysia na Singapore mwaka 1999 na baadaye kuenea katika sehemu zingine za Asia kama Bangladesh na India.

Virusi hivyo viliwasili katikati mwa Malaysia kupitia popo ambao walisimama kula matunda yaliyokuwa yakining'inia juu ya mashamba ya nguruwe. 

Kirusi cha Nipah kiliambukizwa kwa wanadamu kupitia wanyama

Nguruwe walikula mabaki ya chakula hicho cha popo, na virusi vilipitia kwa nguruwe hao kuingia kwa wanadamu waliokuwa wakifanya kwenye mashamba hayo.

Kwa sasa kirusi cha Nipah hakina tiba wala chanjo, na kimekuwa kikijitokeza mara kwa mara katika nchi za Bangladesh na India. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani, asilimia 40 mpaka 75 ya wagonjwa wanaoripotiwa kuwa na kirusi cha Niipah huaga duniani kutokana na kirusi hicho. 

Tags