Oct 17, 2021 12:23 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Umasikini duniani utaendelea kama yasipofanyika mambo matatu

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa umasikiti utaendelea kushuhudiwa duniani endapo walimwengu hawatafanya mambo matatu ambayo anaamini yatasaidia kuondoa umasikini ulimwenguni.

Guterres ametaja mambo hayo kupitia ujumbe wake wa siku ya kutokomeza umaskini dunia, akisema ni hatua ambazo zinapaswa kuleta marekebisho, ujumuishi na uendelevu.

Amesema mambo hayo matatu ni muhimu ili jamii zilizotumbukizwa zaidi kwenye umaskini kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au ziweze kujinasua kwa usalama na kuwa imara zaidi hata baada ya Corona.

Akifafanua mambo hayo matatu ya kujikwamua amesema  kuwa, mosi ni  marekebisho ni muhimu, jambo la pili ni ujumuishi akisema kujikwamua bila usawa ni kuacha nyuma binadamu wengi ambao tayari walikuwa wameenguliwa na hivyo kutofanikisha malengo ya maendeleo endelevu, na jambo la tatu ni uendelevu akisema ni muhimu.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa 

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, COVID-19 imekuwa mwiba katika maisha ya wengi akisema “kwa mara ya kwanza katika miongo miwili, ufukara unaongezeka. Mwaka jana takribani watu milioni 120 walitumbukia kwenye umaskini baada ya COVID-19 kupomorosha uchumi na jamii. Fursa ya kujikwamua nayo inazidisha ukosefu wa usawa kati ya nchi tajiri na maskini. Mshikamano ambao ndio tuna uhitaji zaidi hivi sasa, haupo.”

Mathalani, ukosefu wa usawa kwenye mgao wa chanjo dhidi ya Corona unaruhusu kuchipuka kwa minyumbuliko mipya ya virusi na hivyo kusababisha vifo zaidi na kuongeza udumavu wa uchumi unaogharimu matrilioni ya dola.

Ametaka jamii kutumia siku ya leo na kila siku kushikamana kutokomeza umaskni na kujenga dunia yenye haki, utu na fursa kwa wote.