Oct 19, 2021 02:30 UTC

Video iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii inayomuonesha Rais Joe Biden wa Marekani na mkewe, wakiondoka kwenye mgahawa katika mji mkuu, Washington DC bila ya kuvaa barakoa, imezusha zogo na mjadala mkubwa nchini Marekani.

Kitendo hicho cha Biden na mweke, Jill Biden cha kwenda maeneo ya umma bila ya kuvaa barakoa kimeibua mjadala mkubwa baina ya Wamarekani licha ya kiongozi huyo kusisitiza mara kwa mara kwamba raia wote wanalazimika kuwa na barakoa katika maeneo ya umma katika harakati za kupambana na maambukizi ya kirusi cha corona.

Video hiyo inamuonesha Biden na Jill Biden wakitoka nje ya mgahawa wa kitaliano mjini Washington bila ya kuvaa barakoa. 

Mwezi uliopita Rais wa Marekani alitoa dikrii kwa viongozi wa serikali na makampuni ya binafsi kuhusiana na suala la kuvaa barakoa. Dikrii hiyo inalazimisha kuvaa barakoa katika hoteli na migahawa yote ya Washington DC na mtu yeyote anayekiuka amri hiyo anapigwa faini. 

Marekani inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioambukizwa corona na vilevile idadi ya watu walioaga dunia kutokana na virisi hivyo. 

Karibu Wamarekani laki saba na nusu wameaga dunia hadi sasa kutokana na ugonjwa wa Covid-19