Oct 25, 2021 02:32 UTC
  • Dalali wa silaha za magaidi nchini Syria afilisika, Canada yampa kinga ya ukimbizi

Mmoja wa madalali aliyekuwa akiyauzia silaha magenge ya kigaidi nchini Syria likiwemo la Daesh (ISIS) amefilisika vibaya kiasi kwamba Canada imempa kinga ya ukimbizi nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Ibrahim Kajo, mmoja wa madalali wakubwa wa kuyauzia silaha magenge ya kigaidi nchini Syria likiwemo la Daesh amefilisika kikamilifu kutokana na kudhibitiwa magendo ya silaha na kushindwa nguvu magenge ya kigaidi huko Syria. Hivi karibuni alikimbilia Uturuki na baadaye nchini Canada kupewa ulinzi kwa madai ya mkimbizi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya hapo pia, gaidi huyo mfanya magendo ya silaha alikuwa chini ya uangalizi wa mashirika ya kijasusi ya Uturuki kwa miaka mingi ndani ya Uturuki huku akiwa kiungo muhimu cha kufikishiwa silaha magenge ya kigaidi nchini Syria.

Magaidi wa SDF wanaoungwa mkono kikamilifu na Marekani nchini Syria

 

Jinai za magenge ya kigaidi dhidi ya wananchi na maafisa wa serikali ya Syria ni nyingi sana na zisingelitokea kama si kwa siasa za kibeberu za madola ya Magharibi na vibaraka wao katika eneo la Asia Magharibi.

Katika siku za karibuni jinai za magaidi wanaojiita  vikosi vya kidemokrasia vya Syria (SDF) vimeongezeka sana dhidi ya wakazi wa maeneo yanayoshikiliwa na wanamgambo hao huko kaskazini mwa Syria.

Wanamgambo hao wanaungwa mkono na kufadhiliwa kwa hali na mali na Marekani na wanaipinga serikali halali ya Syria. Wanamgambo wa SDF wametenda na wanaendelea kufanya jinai chungu nzima dhidi ya raia wa Syria. 

Tags