Oct 27, 2021 04:06 UTC
  • Newsweek: Maelfu ya makombora ya Marekani yanayovuka bara yanatishia amani ya dunia

Jarida la Marekani la Newsweek limeashiria ongezeko la vichwa vya nyuklia duniani na kuandika kuwa, maelfu ya makombora ya Marekani yenye uwezo wa kuvuka bara ni tishio kwa amani ya dunia.

Newsweek limeripoti kuwa, idadi ya silaha mpya zilizoundwa na Marekani ni makombora 665 ya balestiki yenye uwezo wa kuvuka bara moja hadi jengine, makombora ya balestiki yanayoongozwa kwa nyambizi chini ya maji na ndege nzito na za kisasa zaidi za kivita, ambazo zote hizo ni tishio kwa amani ya dunia.

Kwa mujibu wa ripoti ya jarida hilo, vichwa 1,389 vya nyuklia vilivyofungwa kwenye makombora ya balestiki yanayovuka bara, makombora ya balestiki yanayoongozwa na nyambizi, vichwa vya nyuklia vinavyobebwa na ndege nzito za kivita na vilevile vifyatuo 800 vya makombora yanayovuka bara, ni miongoni mwa zana za kijeshi zilizomo kwenye orodha hiyo.

Marais wa Russia na Marekani wakati huo, wakisaini mkataba wa New START, Prague Jamhuri ya Czech

Kwa mujibu wa makubaliano ya kupunguza silaha za kushambulia za kistratejia yaliyosainiwa kati ya Russia na Marekani, maarufu kama New START Treaty, kila moja kati ya nchi hizo mbili inapaswa kuhakikisha haimiliki zaidi ya makombora 700 yanayovuka bara, makombora ya balestiki yanayoongozwa na nyambizi na ndege nzito za kivita.

Mkataba wa New START uliosainiwa Aprili mwaka 2010 mjini Prague, Jamhuri ya Czech, ulipigiwa kura na wabunge wa bunge la Russia, Duma mnamo tarehe 27 Januari mwaka huuu wa 2021 kwa anuani ya "Hati ya makubaliano ya kurefusha mkataba wa kupunguza na kuziwekea mpaka silaha za kushambulia za kistratejia baina ya Russia na Marekani", ambapo wabunge hao waliafiki urefushwe tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.../

Tags