Oct 27, 2021 13:01 UTC
  • Wamarekani ni miongoni mwa watu wenye manung'uniko makubwa kwa serikali yao

Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na kituo cha utafiti cha Pew kuhusu nchi zilizoendelea kiuchumi duniani unaonyesha kuwa Wamarekani ni miongoni mwa watu wasioridhishwa na utendaji na wana manung'uniko makubwa kwa serikali yao.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Pew Research Center yanaonyesha kuwa, asilimia 85 ya Wamarekani walioshiriki kutoa maoni yao wanataka yafanyike mabadiliko makubwa katika mfumo wa kisiasa wa nchi yao. Aidha asilimia 76 ya walioshiriki katika uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Pew wanataka mfumo wa huduma za afya ubadilishwe na asilimia 66 wanataka yafanyike mabadiliko ya kiuchumi nchini humo.

Matokeo hayo ya uchunguzi huo wa maoni ambao ulifanywa Februari mwaka huu wa 2012 katika nchi 17 zenye uchumi uliostawi zaidi, yanatolewa katika hali ambayo, mataifa ya dunia yanasokotwa na janga la ulimwengu mzima la maradhi ya Covid-19, hali inayobainisha jinsi janga hilo lilivyoathiri muelekeo na mtazamo wa watu kuhusu demokrasia na mageuzi ya kijamii.

Uvamizi wa jengo la bunge la Marekani

Kwa upande mwingine raia wa nchi 13 kati ya 17 walioshiriki katika uchunguzi wa maoni wa Pew Research Center wametaka yafanyike mageuzi kamili ya kisiasa katika nchi zao, ambapo kwa Italia kiwango cha waliotoa maoni hayo ni asilimia 89 na kwa upande wa Uhispania ni asilimia 86.

Kuhusiana na hali ya uchumi nchini Marekani, matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonyesha kuwa, asilimia 80 ya Wademocrat wanaitakidi kwamba uchumi wa nchi hiyo unahitaji maboresho makubwa, huku asilimia 50 ya Warepublican wakiunga mkono mtazamo huo.../

Tags