Nov 23, 2021 12:08 UTC
  • Msemaji wa UN: Mfumo wa fedha na kibenki wa Afghanistan unakaribia kusambaratika

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine ametahadharisha kuhusu mgogoro wa kiuchumi huko Afghanistan na kueleza kuwa mfumo wa fedha na kibenki wa nchi hiyo unakaribia kuanguka.

Stephane Dujarric amesema kuwa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kuwa, mikopo ya benki ambayo haijalipwa katika soko la hisa huko Afghanistan yameongezeka kutoka asilimia 30 mwishoni mwa mwaka jana wa 2020 na kufikia asilimia 57 mwaka huu.  

Amebainisha kuwa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuendelea kutolewa pesa katika akaunti za benki  kutapunguza amana za benki huko Afghanistan kwa asilimia 40 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2021. 

Mgogoro wa kiuchumi Afghanistan 

Msemaji wa Umoja wa Mataifa aidha ametangaza kuwa, ombi la shirika hilo kwa ajili ya kupatiwa msaada wa fedha wa dola milioni 6.6  ili kuwahudumia watu milioni 11 huko Afghanistan limekidhiwa kikamilifu. 

Uchumi wa Afghanistan umevurugika huku umaskini na ukosefu wa ajira ukiongezeka kufuatia kuanza msimu wa baridi kali. Taasisi za kimatafa pia zimetahadharisha kuwa mgogoro wa kibinadamu huko Afghanistan utasababisha janga kubwa sana la kibinadamu kuwahi kushuhudiwa nchini humo. 

Tags