Nov 27, 2021 04:38 UTC
  • Poland yapunguza uhusiano wake wa kidiplomasia na Israel

Poland imepunguza kiwango cha uhusiano wake wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel, ikisisitiza kuwa serikali ya Warsaw haina mpango wa kutuma balozi mwingine katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

Agosti iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland ilimuita nyumbani balozi wake wa Israel, Marek Magierowski, huku msuguano wa kidiplomasia baina ya pande mbili hizo ukizidi kutokota.

Poland imesema balozi huyo ambaye yuko katika nchi hiyo ya Ulaya kwa ajili ya likizo, hatorejeshwa Tel Aviv, kutokana na kile Warsaw inasema ni 'hatua zisizohalalishika' za utawala haramu wa Israel. Warsaw imebainisha kuwa, imeamua kupunguza kiwango cha uhusiano wake wa kidiplomasia na Tel Aviv, kujibu mapigo ya hatua kama hiyo iliyochukuliwa na Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, sambamba na matamshi yasiyokubalika ya waziri huyo dhidi ya Poland.

Lukasz Jasina, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland amesema hakuna mpango wowote hivi sasa wa kuanzisha mchakato wa kumteua mtu mwingine atakayetwikwa jukumu la kuwa balozi wa nchi hiyo Israel.

Wananchi wa Poland katika maandamano ya kupinga kufidiwa utawala wa Kizayuni

Utawala khabithi wa Israel umekuwa ukiwatuhumu wananchi na serikali ya Poland kuwa walishiriki katika kile kinachodaiwa ni mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Manazi dhidi ya Wayahudi (Holocaust).

Poland ambayo ni moja kati ya nchi zinazotajwa kuwa na kambi zilizotumiwa na Manazi wa Ujerumani wakati wa Holocust, imekanusha tuhuma za kuhusika katika mauaji hayo, sanjari na kupinga suala la kulazimishwa kuupatia fidia utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tags