Nov 27, 2021 08:01 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Mamilioni ya wanawake wanakabiliwa na umasikini kwa sababu ya COVID-19

Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa, janga la ulimwengu la virusi vya Corona limesababisha mamilioni ya wanawake katika maeneo mbalimbali ya dunia kukumbwa na umasikini.

Bi Anita Bhatia, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo, wanawake milioni 55 katika maeneo tofauti ya dunia wanakabiliwa na umasikini uliosababishwa na janga la virusi vya corona.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amebainisha kwamba, katika mataifa yaliyoendelea ambapo wanawake waliowengi wanafanya kazi katika sekta binafsi wamekabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha kufuatia sheria za kukabiliana na msambao wa virusi vya Corona.

 

Kabla ya hapo pia Umoja wa Mataifa ulieleza kuhusu kuweko ubaguzi baina ya wanawake na wanaume baada ya kuibuka viryusi vya Corona.

Wakati huo huo, ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa, nusu ya wanawake duniani ni wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia vitendo ambavyo vinaripotiwa kuongezeka tangu lilipoibuka janga la virusi vya Corona duniani.

Ripoti hiyo imetolewa sambamba na kampeni ya kimataifa ya siku 16 dhidi ya ukatili wa kijinsia iliyoanza Alkhamisi ya 

Aidha ripoti mpya ya Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa iliyoangazia athari za janga la COVID-19 kwa usalama wa wanawake nyumbani na katika maeneo ya umma imeonesha kuwa hisia za usalama za wanawake zimepotea, na kusababisha athari mbaya kwa hali yao ya kiakili na kimihemko.Novemba 25 ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Ukatili Dhidi ya Wanawake.

Tags