Nov 29, 2021 07:12 UTC
  • Michael Cohen: Trump atashindwa tena katika uchaguzi

Aliyekuwa wakili binafsi wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ambaye muda wake wa kutumikia kifungo cha jela umemalizika amesema kuwa iwapo Trump atagombe tena kiti cha urais nchini Marekani basi atashindwa kwa mara nyingine tena.

Michael Cohen wakili wa zamani wa Donald Trump amemkosa vikali Donald Trump  katika mahojiano aliyofanya na televisheni ya BBC. Cohen amesisitiza kuwa moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Trump ni  uwongo mkubwa alioeneza kwamba kura ziliibiwa katika uchaguzi wa rais mwaka jana huko Marekani. 

Wakili wa zamani wa Trump ameongeza kuwa matokeo ya uchaguzi hayakuchakachuliwa. Amehoji: Uwongo huo mkubwa utachukuliwaje iwapo atashindwa tena katika uchaguzi wa 2024? Michael Cohen ametumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukiuka sheria katika masuala ya kifedha, kuwalipa pesa wanawake ambao Trump alikuwa na uhusiano nao wa kingono na kuidanganya Kongresi.  

Cohen aidha atatumikia kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu iliyosalia. Cohen alikiri kuhusu tuhuma zinazomkabili na tuhuma kubwa zaidi kati ya zote ilihusiana na suala la uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 huko Marekani.  

Michael Cohen, aliyekuwa wakili binafsi wa Trump