Nov 29, 2021 07:57 UTC
  • Maduro: Waangalizi wa Umoja wa Ulaya walielekea Venezuela kufanya ujasusi

Rais wa Venezeula amesema kuwa waangalizi wa Umoja wa Ulaya walielekea Venezuela kufanya ujasusi. Amesema walikwenda Venezuela kwa kisingizio cha kusimamia uchaguzi.

Rais Nicolas Maduro amebainsha kuwa waangalizi wa Umoja wa Ulaya ambao walielekea Venezuela eti kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wa Novemba 21 lengo lao lilikuwa ni kufanya ujasusi  nchini humo.

Rais Maduro amesema, ujumbe wa kijasusi wa Umoja wa Ulaya haukupata hata sababu moja ya kukosoa mfumo wa uchaguzi wa Venezuela bali ujumbe huo ulikuwa wa kijasusi na si wa kimataifa. 

Rais Maduro ameongeza kuwa, waangalizi wa Umoja wa Ulaya walikuwa huru huko Venezuela na walifanya ujasusi katika nyuga za maisha ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya wananchi wa Venezuela. Safari ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya huko Venezuela imefanyika kinyume na upinzani wa Marekani kwamba haiitambui rasmi serikali ya Maduro. 

Waangalizi wa EU waliodaiwa kufanya ujasusi Venezuela 

Venezuela tarehe 2 mwezi huu iliendesha uchaguzi wa mabaraza ya miji na serikali za mitaa  ambapo wananchi waliweza kuwachagua viongozi wa vyombo vya utendaji katika serikali za mitaa na wawakilishi wa mabaraza ya majimbo. Chama tawala nchini Venezuela kiliibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi huo na kufanikiwa kupata viti 20 kati ya 23 vya magavana wa majimbo  ya nchi hiyo na pia Meya wa mji mkuu Caracas.