Dec 02, 2021 09:35 UTC
  • Baraza Kuu la UN lazidisha muda wa azimio dhidi ya Israel

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena limetaka kuondoka kikamilifu utawala ghasibu wa Israel katika Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Azimio hilo la leo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeeleza kuwa, uamuzi uliochukuliwa na  Israel Disemba 14 mwaka 1981 wa kulazimisha sheria na kuamua kuikalia kwa mabavu Miinuko ya Golan huko Syria ni batili, usio na itibari na kinyume cha sheria. 

Azimio hilo limesema: Kama ambavyo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilivyosisitiza katika azimio nambari 497 la mwaka 1981, Israel inapaswa kukomesha hatua zake na kuondoka kikamilifu katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Miinuko ya Golan tarehe 4 Juni mwaka 1967.

Nchi 94 wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepiga kura ya ndiyo kwa azimio hilo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bassam Sabbagh amehutubia kikao hicho cha Baraza Kuu la UN na kusema mwenendo wa sasa wa Umoja wa Mataifa wa kutotekeleza maazimio yake unaushajiisha utawala ghasibu wa Israel kuendeleza uvamizi na ukanzamizaji dhidi ya raia wa Syria katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Golan.

Miinuko ya Golan Syria inayokaliwa kwa mabavu na Israel 

Sabbagh ameongeza kuwa, Syria inautaka Umoja wa Mataifa uchukue hatua madhubuti zaidi na za kivitendo kwa ajili ya kutekeleza maamuzi yake na kukomesha kukaliwa kwa mabavvu eneo la Golan la ardhi nyingine zinazokaliwa kwa mabavu na Israel. 

Ameema Syria inalinda haki yake ya kukomboa ardhi hiyo ya Golan na kwamba haitafanya mazungumzo ya aina yoyote kuhusiana na haki hiyo.         

Tags