Dec 04, 2021 02:38 UTC
  • Borell na Abdullahiyan: Anga ya mazungumzo ya Vienna ni chanya

Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran wamewasiliana kwa njia ya simu na kuyatathmini mazungumzo ya kuondoa vikwazo yanayoendelea mjini Vienna, Austria kuwa ni chanya.

Josep Borrel Mkuu wa wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Mratibu wa mazungumzo ya Vienna jana alizungumza kwa njia ya simu na Hussein Amir Abdollahiyan Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kuhusu mchakato wa mazungumzo hayo.

Borell amezitaja juhudi za Ujerumani, China, Russia, Ufaransa, Uingereza na hususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kufikia mapatano huko Vienna kuwa muhimu na kueleza kuwa amemtaka Enrique Mora Katibu Mkuu wa kitengo cha External Action Service cha EU kufanya juhudi kubwa na kuishirikiana na Mkuu wa Timu ya Mazungumzo ya Iran na jumbe zote husika ili kufikia mapatano. 

Katika mazungumzo hayo ya simu, Hussein Amir Abdollahiyan ameutaja mchakato wa mazungumzo ya Vienna kuwa mzuri kwa ujumla lakini unaokwenda taratibu na kueleza kuwa, ujumbe wa Iran unashiriki kikamilifu mazungumzo ya Vienna kwa njia njema, kwa matarajio ya kufikiwa mapatano.

Kikao cha pamoja kati ya Iran na kundi la 4+1 

Wakati huo huo Hussein Amir Abdollahiyan amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendeleza ushirikiano  wa kiufundi na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Vienna tayari  umewasilisha rasimu mbili za mapendekezo yake kwa kundi la 4+1 katika fremu ya masuala mawili yaani kuondoa vikwazo vya kidhalimu na suala la nyuklia. 

Tags