Dec 14, 2021 09:57 UTC
  • China: Kizoro cha dai la demokrasia kimefunuka, sura halisi ya Marekani imefichuka

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema, Marekani haiwezi tena sasa kuwababaisha na kuwapotosha watu.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Wang Wenbin amekosoa kongamano la demokrasia lililofanyika hivi karibuni nchini Marekani na akaeleza kwamba: kizoro ilichokuwa imejifunika nchi hiyo inayojinadi kuwa mtetezi wa demokrasia kimefunuka na sura halisi na haribifu ya Marekani imewadhihirikia watu wote.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amefafanua kwamba,"ni watu wachache katika mitandao ya kijamii waliovutiwa na kurushwa hewani moja kwa moja kongamano hilo, lakini video iliyoonyesha uingiliaji kijeshi wa Marekani na mauaji iliyofanya ya raia imeangaliwa na watu wengi, jambo linaloonyesha kuwa juhudi za Washington za kutaka ionekane mtetezi wa demokrasia hazijapewa umuhimu na watu.

Wang Wenbin

Hivi karibuni, Marekani iliitisha kongamano la demokrasia mjini Washington, wakati kwa mtazamo wa wataalamu wa masuala ya kimataifa na hata maafisa waandamizi wa ndani ya nchi hiyo demokrasia ya Kimarekani inaendelea kumomonyoka.

Kwa upande mwingine, miaka 20 iliyopita, Marekani na waitifaki wake waliivamia kijeshi na kuikalia kwa mabavu Afghanistan kwa kisingizio cha kuiletea uhuru na demokrasia ya Magharibi, lakini hatimaye, mbali na kukiri kuwa hawakuweza kulifikia lengo hilo, walifunga virago na kuikimbia nchi hiyo.../

Tags