Dec 23, 2021 08:08 UTC
  • India yawapatia uraia wasio Waislamu kutoka Afghanistan, Pakistan na Bangladesh

Serikali ya India imesema imewapatia uraia watu elfu tatu, ambao ni raia wa jamii za wachache katika nchi za Afghanistan, Pakistan na Bangladesh.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Nityanand Rai ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba, maombi ya uraia iliyopokea wizara yake kutoka kwa watu wa jamii za wachache za Wahindu, Makalasinga na Wakristo katika nchi za Pakistan, Bangladesh na Afghanistan katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imefika 8,244.

Kwa mujibu wa Rai, kati ya watu hao, 3,117 wameshapatiwa uraia wa India.

Narendra Modi

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, mwezi Juni 2019, utawala wa waziri mkuu wa India Narendra Modi ulitangaza kuwa, utawapatia uraia wakimbizi wasio Waislamu wanaosumbuliwa kwa sababu za kidini katika nchi hizo tatu. Hata hivyo vyama vya siasa na asasi za kiraia nchini India zimeulalamikia uamuzi huo na kusema kuwa ni wa kibaguzi, kwa sababu hautoi fursa ya kunufaika na sheria hiyo wakimbizi Waislamu wanaonyanyaswa katika nchi zingine.../

Tags