Dec 30, 2021 11:39 UTC
  • Uchoraji tattoo wapigwa marufuku kwa wachezaji wa soka nchini China

Viongozi wa michezo nchini China wamesema, kutokana nyota wa mchezo wa soka kuwa ni kigezo na mfano wa kuigwa kwa vizazi mbalimbali, ni marufuku kwa wachezaji hao kujichora tattoo.

Uchoraji tattoo ni mtindo uliozoeleka kwa wanamichezo wa fani mbaimbali hasa nyota wa mchezo wa mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, kwa kuzingatia mitazamo tofauti iliyopo juu ya suala la malezi na makuzi ya vizazi vijavyo, serikali za nchi mbalimbali zimekuwa na mitazamo inayotofautiana kuhusu namna ya kuamiliana na mtindo huo wa uchoraji tattoo.

Katika mchezo wa soka nchini China mamlaka husika zimechukua hatua kali za kukabiliana na uchoraji tattoo ambapo kwa mujibu wa ripoti, mlinzi wa timu ya taifa ya nchi hiyo Zhang Linping ametakiwa afiche tattoo zake wakati anapokuwa katika timu ya taifa na klabu yake ya Guangzhou.

Kwa mujibu wa agizo lililotolewa na maafisa wa michezo wa China, uchoraji tattoo ni marufuku pia kwa wachezaji wa soka wa timu za umri chini ya miaka 20.../

 

Tags