Jan 04, 2022 07:59 UTC
  • Barua za chuki dhidi ya Uislamu zasambazwa misikitini Uholanzi

Wakfu wa Dini Uholanzi umelaani vikali kitendo cha kusambazwa barua zenye jumbe za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika misikiti kadhaa ya nchi hiyo ya Ulaya.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na waqfu huo imeeleza kuwa, mbali na barua za chuki, lakini misikiti hiyo ya Uholanzi wiki iliyopita ilipokea pia picha zenye vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW). 

Wakfu wa Dini Uholanzi imezitaka mamlaka husika za nchi hiyo kuwatambua na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu na jamii ya Waislamu wa nchi hiyo.

Wakfu huo ambao uliasisiwa miaka 40 iliyopita nchini Uholanzi, umesisitiza kuwa unalaani vitendo vyote vya kuyavunjia heshima matukufu ya kidini.

Msikiti Uholanzi ulivyoteketezwa moto na wenye chuki miaka kadhaa nyuma

Mwaka 2005 gazeti la Kiholanzi la Jyllands-Posten lilisambaza vibonzo vyenye kumvunjia heshima Nabii Muhammad (SAW) suala lililoibua maandamano makubwa ya kulaani kitendo hicho kote duniani.

Aidha Agosti mwaka 2019, uvaaji wa vazi la burqa linalotumiwa na baadhi ya wanawake wa Kiislamu ulipigwa marufuku katika maeneo ya umma na vyombo vya usafiri nchini Uholanzi kwa kuanza kutekelezwa rasmi sheria hiyo.

 

Tags